Katibu wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni nchini Iran amesema hayo katika mkutano wa kutiwa saini mkataba wa ushirikiano kati ya baraza hilo na Maktaba ya Taifa ya Iran. Muhammad Reza Muhbirdezfuli amesema kuwa huko nyuma, maktaba ilijulikana kama “Baitul Hikma” au nyumba ya hekima.
Amesema ustaarabu wa Kiislamu uliweza kunawiri kupitia nyumba hizo za hekima. Muhbirdezfuli amesema wasomi bingwa katika zama za kunawiri ustaarabu wa Kiislamu walitekeleza majukumu yao katika kuimarisha na kustawisha maktaba. Amesema maktaba ya Taifa ya Iran inapaswa kuchukua vigezo kutoka wasomi hao wa kale.
Naye Ali Akbar Ashaari Mkuu wa Maktaba ya Taifa ya Iran ambaye pia ni Mshauri wa Rais amesema kuna haja ya uwezo wa taasisi mbalimbali kujumuishwa kwani ushirikiano kama huo ni kwa maslahi ya ustawi kisayansi na kielimu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 396844