IQNA

Uzingatiwaji utamaduni umefanikisha sinema Iran

15:46 - April 30, 2009
Habari ID: 1771856
Mafanikio makubwa zilizopata sinema zilizozalishwa Iran katika tamasha za sinema za Russia ni jambo linaloashiria mitazamo ya pamoja ya nchi hizi mbili katika masuala ya utamaduni.
Mwandishi wa IQNA amemnukulu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Muhammad Hussein Safar Harandi akiyasema hayo alipokutana na mwenzake wa Russia mjini Moscow ambapo pia ameashiria kufanyika kwa mafanikio maonyesho ya Wiki ya Utamaduni ya Iran na Russia katika nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa Iran inataka wachapishaji vitabu wa Russia kushiriki katika maonyesho yajayo ya kimataifa ya vitabu ya Tehran.
Aidha amesema nchi hizi mbili zinapaswa kujitahidi kufasiri vitabu vya fasihi vya wasomi bingwa.
Naye Alexander Avdeev Waziri wa Utamaduni wa Russia amesema Iran ni moja kati ya marafiki muhimu zaidi wa Russia. Amesema watu wa Russia wanaupenda utamaduni na ustaarabu wa Iran. Ameongeza kuwa nchi yake inataka kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni na Iran.
Waziri wa Utamaduni wa Russia ameelezea wasi wasi wake kutokana na hujuma ya utamaduni wa Magharibi nchini Russia na kusema: “Ingawa kuna baadhi ya nukta chanya katika ustaarabu wa Magharibi lakini Russia inapinga kuingizwa nchini humo utamaduni wa Kimarekani ambao unavuruga thamani za kimaadili”. 396829
captcha