Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia SPA, kikao hicho kimefanyika kwa ushirikiano wa jumuiya iliyotajwa na Muungano wa Kiislamu wa Benin. Maimamu wa swala ya Ijumaa na wakuu wa jumuiya za Kiislamu za Benin wameshiriki katika kikao hicho na kubadilishana mawazo kuhusiana na njia za Waislamu kuishi pamoja kwa amani, kuheshimiana na kusameheana.
Akiwa katika safari ya kuzitembelea nchi kadhaa za Kiafrika at-Turki siku ya Ijumaa alivitembelea vituo kadhaa vya Kiislamu na utafiti vya Niger na pia kuitembelea misikiti kadhaa ya nchi hiyo. Siku ya Jumamosi pia alionana na kuzungumza na Is'haq Labou, Waziri wa Niger anayeshughulikia Masuala ya Kidini na Huduma za Kibinadamu na hatimaye kukitembelea Kituo cha Kiislamu cha Mfalme Faisal mjini Niamey, mji mkuu wa Niger. Akiwa nchini humo, ameonana pia na Rais wa Niger, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge la nchi hiyo. Pia amefungua Kituo cha Kiutamaduni na Kiislamu cha Amir Salman nchini humo.
Baada ya Niger, at-Turki anatazamiwa pia kuzitembelea nchi za Sierra Leone, Chad na Djibouti na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hizo pamoja na wa misikiti na jumuiya za Kiislamu na vilevile kuchunguza hali ya Waislamu katika nchi hizo. 398056