Sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa), nembo ya mapambano na subira, zimefanyika katika Kituo cha Kiislamu nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa ripoti ya kituo hicho, washairi mashuhuri wameshiriki katika sherehe hizo na kusoma mashairi ya kumsifu Bibi Zainab (sa).
Ummu Mahdi al-Musawi, mmoja wa wanawake mashuhuri wahubiri wa Kishia nchini Uingereza na al-Haj Uruba Mudlij, hatibu mwingine mashuhuri wa Kishia nchini Uingereza, wameshiriki katika sherehe hizo na kutoa hutoba kuhusiana na maisha na mfano mzuri wa bibi Zainab (sa) kwa Waislamu na hasa kwa tabaka la wanawake.
Bibi Zainab Kubra (sa) alizaliwa tarehe Tano Jamadil Awwal na kusomeshwa masomo ya Kiislamu na mama yake mtukufu Bibi Fatuma (as), binti ya Mtume Muhammad (saw). 398092