IQNA

Kitabu cha usanifu majengo katika Ustaarabu wa Kiislamu chachapishwa na ISESCO

8:46 - May 04, 2009
Habari ID: 1773465
Kitabu kiitwahco, ‘Usanifu Majengo Katika Ustaarabu wa Kiarabu na Kiislamu’ kimechapishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Kuwait KUNA, kitabu hicho kimeandikwa na Badie Al Abid mtaalamu wa utamaduni na sanaa katika shirika la ISESCO.
Katika utangulizi wa kitabu hjicho, mwandishi anasema kuwa kinyume na nchi za Magharibi , usanifu majengo katika ustaarabu wa Kiislamu na Kiarabu una ufahamu wa siku nyingi na asili ambao misingi yake iko katika sheria na falsafa ya ustaarabu wa Kiislamu.
Shirika la ISESCO linazingatia sana suala la usanifu majengo wa Kiislamu na hadi sasa kuna vitabu kadhaa vilivyochapishwa na shirika hilo kuhusiana na maudhui hii ambavyo ni pamoja na, ‘Njia za Ustawi wa Sanaa za Usanifu Majengo wa Kiislamu’, ‘Sanaa ya Usanifu Majengo wa Kiislamu katika eneo la Balkan’ na ‘Sanaa za Usanifu Majengo wa Kiislamu na Sifa Zake Maalumu katika Mbinu za Mafunzo’. 398358
captcha