IQNA

Rais Mahmoud Ahmadinejad:

Mfumo wa sasa duniani ni wa kidhalimu

8:22 - May 04, 2009
Habari ID: 1773471
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mfumo ambao umekuwa ukitawala dunia katika kipindi cha miaka 100 iliyopita hauwezi kutatua matatizo mbalimbali ya ulimwengu.
Akizungmza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Hirofumi Nakasone mjini Tehran, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa mfumo unaotawala dunia una sifa na misingi ya kidhalimu. Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kushirikiana na Japan katika kuanzisha mfumo wa kiadilifu duaniani.
Rais Ahmadinejad amautaja uhusiano wa Iran na Japan kuwa wa kirafiki na kuongeza kuwa mataifa haya mawili ni vitovu vya utamaduni na ustaarabu na kwamba staarabu za nchi hizi mbili zina nukta nyingi za pamoja.
Rais Ahmadinejad amesisitiza kuwa sera za Iran ni kuwa na uhusiano huru na nchi nyinginezo duniani bila kuathiriwa na mitazamo ya wengine. Rais wa Iran ameashiria matukio makubwa ambayo yatajiri katika siku za usoni duniani na kusema kuwa mfumo ulioibuka baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia umefika ukingoni.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan ameashiria sifa za kipekee za kihistoria za ustaarabu wa Iran na kusema kuwa nchi yake inataka kuimarisha ushirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema Iran ni dola lenye nguvu kieneo na lenye historia ya siku nyingi. 398744
captcha