Dr. Garjian wa Chuo Kikuu cha Baqir Ulom amesema Shahid Mutahhari aliendesha shughuli zake zote kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu na kwa hivyo daima ataendelea kukumbukwa.
Ameongeza kuwa Ustadh Mutahhari hakuwa mtu wa zama maalumu bali fikra zake zinavinufaisha vizazi vyote.
Dr. Garjian amesema Shahid Mutahhari alifahamu vyema jinsi ya kusoma na kutekeleza kivitendo aliyojifunza na kwamba alitafuta elimu kwa moyo wenye ikhlasi.
Amezitaja sifa za kipekee za Shahid Mutahhari kuwa ni pamoja na kufungamana kikamilifu na Qur'ani Tukufu, uzingatiaji wa kina wa Sala, ushujaa na kadhalika.
Dr. Garjian amesema harakati muhimu za Shahid Mutahhari zilijumuisha kupambana dhidi ya sumu ya Umagharibi na kuhuisha Uislamu. Ameongeza kuwa Shahid Mutahhari kwa alichukua muda mrefu kufanya utafiti kabla ya kuendea kutoa muhadhara.
Vitabu vya Shahid Mutahhari vinaendelea kuwavutia wengi duniani na hivyo kuzidisha haja ya kufasiriwa kwa lugha mbalimbali. 399159