IQNA

11:44 - May 06, 2009
Habari ID: 1774771

Tehran kuwa mwenyeji wa semina ya kimataifa ya "Mwanamke katika Historia ya Kiislamu"

Semina ya nne ya kimataifa ya Mwanamke katika Historia ya Kiislamu imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu mjini Tehran. Semina hiyo itasimamiwa na Jumuiya ya Wanawake Watafiti wa Historia ya Iran.

Katibu wa semina hiyo Nuzhat Ahmadi ametoa ripoti kuhusu semina tatu zilizotangulia na kusema kuwa Jumuiya ya Wanawake Watafiti wa Historia imekusudia kujadili suala la wanawake katika vipindi mbalimbali na katika fikra na uchunguzi wa wasomi.
Semina hiyo pia itachunguza nafasi ya mwanamke nchini Iran, nafasi ya mwanamke katika historia ya sasa, na nafasi ya mwanamke katika historia ya Uislamu tangu mwanzoni mwa kudhihiri dini hiyo hadi wakati wa mashambulizi ya Mogul.
Bi Nuzhat Ahmadi amesema kuwa lengo kuu la semina hiyo ni kuweka wazi nafasi ya mwanamke katika dini ya Kiislamu na kujenga uhusiano wa kudumu kati ya wanaharakati wa kike katika uwanja huo.
Amesema kuwa mchango wa wanawake katika historia ya Kiislamu unahitaji uchunguzi mkubwa na wa kina na kwamba suala hilo litasaidia kutambua nafasi yao katika masuala ya kijamii ya zama hizi. 400177

captcha