Kwa mujibu wa Gazeti la Al Sharq al Ausat, Ehsanoglu amesema pendekezo la msaada huo litawasilishwa rasmi katika kikao kijacho cha mawaziri wa mambo ya nje wa OIC kitakachofanyika Damascus Syria.
Ameongezka kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ina mpango wa zaidi ya dola milioni mia moja kwa ajili ya kulijenga upya eneo la Ghaza ambalo liliharibiwa katika hujuma ya kinyama ya utawala haramu wa Israel.
Ehsanoglu ameongeza kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu imefanikiwa kukusanya misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya Wapalestina wanaopata masaibu huko Ghaza. Ameongeza kuwa OIC inashirikiana na Jumuiya ya Hilali Nyekundi ya Palestina pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi Wapalestina UNRWA ili kuwasaidia watu wa Ghaza.
Katibu Mkuu wa OIC amesema hujuma ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ghaza ilisababisha mkasa mkubwa wa kibinaadamu. Amesema hujuma hiyo ya kinyama na iliyo kinyume cha maadili ya ubinaadamu ya Wazayuni imewawekea wazi walimwengu utambulisho halisi wa kikatili wa Israel. 401547