IQNA

Jordan yatia saini mkataba na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu

23:31 - May 10, 2009
Habari ID: 1776599
Serikali ya Jordan imetia saini mapatano ya ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu IDB.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Jordan, sherehe za utiwaji saini mapatano haya mjini Amman zimehudhuriwa na Dr. Ahmad Mohammad Ali Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu na Sahir al Ali Waziri wa Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jordan.
Mapatano hayo yana thamani ya Dola Milioni 10 .7 na yanakusudia kuimarisha uwekezaji wa Kiislamu na kueneza ushirikiano kati ya serikali ya Jordan na IDB.
Lengo la mapatano hayo limetajwa kuwa ni kuunga mkono uwezo wa uwekezaji katika mfuko wa maendeleo, kubuni nafasi za ajira Jordan na kuimarisha uwekezaji wa Kiislamu katika taasisi ndogo ndogo.
Misaada ya IDB kwa Jordan tokea mwaka 1974 hadi sasa ni dola milioni 700.
402731
captcha