IQNA

12:30 - May 12, 2009
Habari ID: 1777345

Abdullah al-Turki atunukiwa nishani ya "Huduma kwa Waislamu na Uislamu"

Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti amemtunuku Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu Duniani (Muslim World League) Dr. Abdullah bin Abdul Mohsin Al-Turki nishani ya "Huduma kwa Waislamu na Uislamu".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kuwait Rais Omar Guelleh siku ya Jumatatu amehutubu katika sherehe za kutunuku nishani hiyo na kusema: "Nishani hii ni nembo kutoka serikali ya Djibouti ya kutoa shukrani Jumuiya ya Kiislamu Duniani kwa juhudi zake za kuwahudumia Waislamu na kujenga vituo maalumu katika maeneo ambayo Waisalmu ni wachache duniani".
Kwa upande wake Dr. Abdullah bin Abdul Mohsin Al-Turki amesema hivi karibuni amezitembelea nchi kadhaa za Kiafrika zikiwemo Benin, Chad, Senegal, Sierra Leone na Djibouti na kuhudhuria vikao na mitano mbali mbali kwa lengo la kujadili hali ya Waislamu barani Afrika. 403399

captcha