Akizungumza hivi karibuni mbele ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, Dalai Lama amekosoa vikali utumiaji mbaya wa jihadi ya Kiislamu na kuongeza kuwa kila mtu anayeelewa vyema sheria za Kiislamu anafahamu kwamba jihadi ina maana ya kujitetea. Amesema katika miaka ya hivi karibuni jihadi imekuwa ikitumiwa vibaya zaidi ulimwenguni kuliko jambo jingine lolote. Dalai Lama pia amesisitiza kwamba neno 'Allah' na kumsifu Mwenyezi Mungu lina maana ya mahaba na mapenzi makubwa yasiyo na mwisho na kwamba Uislamu unawafundisha wafuasi wake kuwapenda wanadamu wote wawe, ni Waislamu au la.
Katika maandishi yake pia, Karen Armstrong, mwandishi mashuhuru wa Uingereza kuhusiana na masuala ya dini za mbinguni, amekosoa vikali upotoshaji na matumizi mabaya ya neno jihadi katika nchi za Magharibi na kusisitiza kwamba upotoshaji huo unafanywa makusudi kwa madhumuni ya kufikia malengo maalumu. 403367