IQNA

16:18 - May 14, 2009
Habari ID: 1778336

Wahubiri watakiwa kuzungmza kuhusu thamani za familia katika Uislamu

Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan imetoa wito kwa mahatibu na wahubiri kuzungmza zaidi kuhusu nafasi ya familia katika Uislamu na wasisitize kuhusu thamani za Kiislamu katika familia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Jordan, wizara hiyo imewataka mahatibu wa Misikiti, Maimamu wa Jamaa na Ijumaa na wahubiri kutumia mimbar kueneza mafundisho ya Kiislamu kuhusu Uislamu. Aidha amewataka kuzungmza kuhusu athari mbaya za kutumia mabavu katika familia. Maagizo hayo mapya ya Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan yametolewa kwa ushirikiano na Baraza la Kitaifa la Familia. Hatua za wizara hiyo zinachukuliwa kwa sababu Mke wa Mfalme wa Jordan, Malikia Rania Abdullah anaongoza mikakati na kukabiliana na mabavu na hujuma dhidi ya wanawake na watoto katika familia. 404281


captcha