IQNA

Kitabu cha 'Uislamu na Mazingira' kwa lugha za Kifarsi, Kiarabu na Kiingereza

16:19 - May 14, 2009
Habari ID: 1778337
Kitabu cha 'Uislamu na Mazingira' kilichoandikwa na Ayatullah Jawad Amuli wa Iran kimecapishwa kwa lugha za Kifarsi, Kiingereza na Kiarabu na kinauzwa katika maonyesho ya 21 ya vitabu Tehran.
Katika kitabu hicho chenye sura tano mwandishi anaelezea masuala mbali mbali yanayoshusiana na mazingira na msimamo wa Kiislamu kuhusiana na suala hilo.
Kitabu hicho kimechapishwa na Taasisi ya Asrar ambayo imewasilisah zaidi ya vitabu 100 katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya Tehran. Ayatollah Javad Amoli ni moja kati ya wanazuoni maarufu nchini Iran mwenye makao yake katika mji wa Qum na ameandika vitabu vingi sana mbali na kutoa mihadhara mara kwa mara katika televisheni na radio.404579

captcha