IQNA

11:51 - May 21, 2009
Habari ID: 1781008

Wamagharibi wasitekeleze siasa za kindumakuwili kuhusu masuala ya Kiislamu

Muhammad as-Shahat al-Jundi, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Cairo, amesema kuwa kufanikiwa kwa mazungumzo kati ya nchi za Magharibi na Ulimwengu wa Kiislamu kunahitajia heshima ya pande mbili na kuzitaka jamii za Magharibi kutochukua misimamo ya kundumakuwili kuhusiana na masuala ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, mazungumzo kati ya Magharibi na ulimwengu wa Kiislamu yanapaswa kufanyika kwa msingi wa kuimarisha uhusiano mwema na kwa madhumuni ya kuheshimiana na kufahamiana pande mbili. Al-Jundi amezitaka nchi za Kiislamu kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wao na jamii pamoja na jumuiya za Kiislamu zinazoishi katika nchi za Ulaya na Marekani ili kukabiliana na mielekeo iliyo dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi. Al-Jundi amesisitiza mwishoni juu ya udharura wa kuanzishwa televisheni ya satalaiti kwa madhumuni ya kutangaza matangazo na vipindi vya Kiislamu ili kuwafahamisha raia wa nchi za Magharibi mafundisho halisi ya Kiislamu. 407641
captcha