IQNA

11:55 - May 21, 2009
Habari ID: 1781117

Kogamano la 'Imam Khomeini (SA) na Umoja wa Waislamu' kufanyika Malaysia

Kongamano la "Athari ya Fikra za Imam Khomeini (SA) katika Umoja wa Waislamu" litafanyika Kuala Lumpur Malaysia kwa munasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 20 wa kuaga dunia Imam Khomeini (SA).

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limeandaliwa na Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mayalsia. Kongamano hilo litajadili masuala kama vile 'Mifarakano inayozushwa na makundi ya Kiwahabbi na Udharura wa kukabiliana na makundi hayo yaliyo dhidi ya Uislamu', 'kueneza fikra za Imam Khomeini (SA) kuhusu umoja wa Kiislamu', 'kujadili kuhusu utamaduni wa umoja', na 'kutoa muongozo kwa jamii za Kiislamu kuhusu mbinu za kusambaratisha njama za maadui'. 408220
captcha