Geert Wilders, mbunge mwenye misiamamo ya kupindukia mipaka dhidi ya Uislamu wa Uholanzi na mtengenezaji wa filamu ya matusi na dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu ametangaza kuwa atashiriki katika maandamano yajayo yaliyo dhidi ya Uislamu yaliyopangwa kufanyika nchini Marekani tarehe 11 Septemba mwaka huu ili kuonyesha mfungamano wake na wapinzani wa Uislamu nchini humo.