Kongamano hilo linatazamiwa kufanyika tarehe 20/21 Septemba na litahudhuriwa na wasomi kutoka maeneo mbali mbali ya dunia. Washiriki watachunguza nafasi ya kisiasa ya wanawake Waislamu katika jamii za Uingereza, Ufaransa na nchi nyingine kubwa duniani.
Masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na kushiriki wanawake Waislamu katika shughuli za kijamii na kisiasa katika nchi zisizo za Kiislamu hasa Uingereza na Ufaransa, njia za kuimarisha ushirikiano baina ya wanaharakati wanawake Waislamu na mashirika ya kutetea haki za wanawake.
629394