IQNA

Qatar kukaribisha wasomaji mashuhuri wa Qur'ani katika mwezi wa Ramadhani

19:06 - August 10, 2010
Habari ID: 1970916
Idara ya Ulinganiaji na Muongozo pamoja na Idara ya Misikiti inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar zitakuwa wenyeji wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Gazeti la ar-Raya la nchini Qatar limeandika kuwa wasomi hao wa Qur'ani wamealikwa nchini humo ikiwa ni katika juhudi za kuhuisha thamani za mwezi wa Ramadhani kupitia usomaji Qur'ani. Gazeti hilo limeendelea kusema kuwa kualikwa kwa wasomoji Qur'ani mashuhuri wa Kiislamu nchini humo kunatimia katika juhudi za kuimarisha nafasi ya Qatar katika kushughulikia masuala ya Qur'ani na kidini nchini katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Mbali na shughuli ya usomaji Qur'ani ratiba nyingine mbalimbali za kidini na kiutamaduni zitatekelezwa pembeni mwa shughuli hiyo. Licha ya hayo wanazuoni na wahubiri wa Kiislamu pia watapewa fursa ya kutoa mawaidha kuhusiana na fadhila za mwezi huu mtukufu. 630288
captcha