IQNA

Maonyesho ya athari nadra za sanaa ya Kiislamu Dubai

19:18 - August 17, 2010
Habari ID: 1975772
Athari za sanaa nadra za kale za Kiislamu zinaonyeshwa katika Kituo cha Kimataifa cha Masuala ya Fedha cha Dubai kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza nchini Imarati yanajumuisha athari 99 za sanaa ya Kiislamu.
Pazia la kaburi la Mtume Muhammad (saw) katika kipindi cha mwanzoni mwa karne ya 19 ambalo liliyatayarishwa kwa amri ya Sultan Mahmoud wa Pili mtawala wa Kiothmani na kipande cha jiwe la mihrabu ya msikiti uliojengwa katika karne ya 10 ni miongoni mwa athari za kisanii zilizoko katika maonyesho.
Maonyesho hayo yalifunguliwa Jumapili iliyopita na Waziri wa Elimu wa Imarati Sheikh Nahyan bin Mubarak na yataendelea katika mwezi mzima wa Ramadhani. 635434
captcha