IQNA

11:36 - August 22, 2010
Habari ID: 1978229

Mbinu za Kuhifadhi Qur'ani zawasilishwa katika maonyesho ya Qur'ani

Mbinu mpya zaidi ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Iran ijulikanayo kama “Hifadhi Qur'ani kwa Njia ya Simu” imewasilishwa katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kuna mpango wa masomo ya miaka miwili, mitatu na minne kwa wanaotaka kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Kwa mujibu wa mpango huo Maustadhi wa Taasisi ya Darul Qur'an ya Iran watakuwa wakipiga simu kwenye nyumba za washiriki na kwa njia hiyo kutoa mafunzo ya kuhifadi Qur'ani Tukufu.
Washiriki watahifadhi Qur'an kwa mujibu wa sura na watasahihishwa makosa yao na kusaidiwa kuhifadhi Qur'ani kwa njia rahisi. 638413
captcha