IQNA

14:04 - August 26, 2010
Habari ID: 1981656

Uturuki yaandaa kikao cha 'Matatizo ya Zama na Utatuzi wa Kiislamu'

Kikao cha 'Matatizo ya Zama Hizi na Utatuzi wa Kiislamu' kinafanyika leo Alkhamisi tarehe 26 nchini Uturuki.

Kikao hicho kimeandaliwa na idara ya masuala ya utamaduni ya meya wa mji wa Istanbul pamoja na idara ya kuadhimisha mji huo kama mji mkuu wa utamaduni wa Ulaya katika mwaka huu wa 2010. Kikao hicho kitawashirikisha wageni wengi waalikwa akiwemo Abdul Hakim Murad, mhadhiri wa masuala ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza, wanachama wa kamati ya kuadhimisha mji wa Istanbul kama mji mkuu wa utamaduni wa Ulaya katika mwaka wa 2010 pamoja na idadi kubwa ya wasomi na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Uturuki. Kikao hicho kinafanyika katika ukumbi wa maktaba ya serikali ya Beyazit katika mji wa Istanbul.
Mazungumzo kuhusu dini na ukisasa, uhusiano kati ya Uislamu na Ukristo, mafundisho ya Kiislamu, utatuzi wa matatizo ya mwanadamu na maadili ya Kiislamu katika mtazamo wa Qur'ani Tukufu ni baadhi ya masuala muhimu yatakayochunguzwa katika kikao hicho. Tomothy Winter anayejulikana kwa jina mashuhuri la Kiislamu la Abdul Hakim Murad ni muhadhiri wa masuala ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Mkuu wa Chuo cha Utafiti cha Wolfoson, Katibu wa Chuo cha Kiislamu cha Muslim Academic Trust mjini London na Mkuu wa Jamii ya Waislamu wenye asili ya Uingereza katika Ulaya ya Magharibi. Msomi huyo pia ni mjumbe wa kamati ya urafiki ya Uingereza na Bosnia Herzegovina. 641515
captcha