IQNA

11:16 - August 29, 2010
Habari ID: 1983187

India, mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha Maelewano na Ushirikiano wa Kidini Duniani

Kikao cha kimataifa cha Maelewano na Ushirikiano wa Kidini Duniani kimepangwa kufanyika tarehe 11 hadi 13 za mwezi Disemba huko Calcutta nchini India.

Kikao hicho kimeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Utafiti wa Kijamii na Kidini IFSSR. Jumuiya hiyo imesema kikao hicho kitawashirikisha wanafikra na wataalamu wa masuala ya kijamii, viongozi na wanazuoni wa dini tofauti ulimwenguni kwa ajili ya kunyanyua kiwango cha utamaduni wa kufanyika mazungumzo chanya ya kuimarisha maelewano miongoni mwa wafuasi wa dini tofauti duniani.
Maudhui kama vile, dini chanzo cha umoja, amani ya dunia katika kivuli cha ushirikiano wa dini na mbinu za kukabiliana na hitilafu za kidini ulimwenguni ni baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho cha kimataifa.
Walio na hamu ya kushiriki katika kikao hicho wanaombwa kuwasilisha makala zao kwa sekretarieti ya kikao hicho tokea tarehe 22 mwezi Novemba. 643337
captcha