IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Misri yaanza

14:26 - September 06, 2010
Habari ID: 1988593
Mashindano makubwa ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Misri yameanza yakiwashirikisha watu 300 katika mkoa wa Matruh.
Kwa mujibu wa tovuti ya ndp.org.eg, mashindano hayo yanafanyika kwa himaya ya Makao Makuu ya Chama cha Kidemokrasia NDP ambacho ni chama tawala cha Misri na yataendelea kwa siku mbili. Mashindano hayo yalianza Jumapili kwa hotuba ya Ali Kheirullah Fadhil Katibu Mkuu chama cha NDP mkoani Matruh.
Mashindano hayo yatakuwa katika viwango vya kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 15 na juzuu 7.
648870
captcha