IQNA

Ufaransa kuanda vikao kadhaa kuhusu hija

11:50 - September 07, 2010
Habari ID: 1989353
Mji mkuu wa Ufaransa Paris utakuwa mwenyeji wa vikao kadhaa vitakavyojadili masuala mbalimbali kuhusu hija.
Vikao hivyo ambavyo vimeandaliwa na Chuo cha Hija cha Paris vimepangwa kuanza tarehe 18 Septemba. Kwa mujibu wa Saphirnews lengo la kufanyika vikao hivyo vya Kiislamu ni kutoa mafunzo ya kutosha kuhusiana na utekelezaji wa hija kwa mahujaji wanaoazimia kuzuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu mwaka huu na kuzungumzia ibada zinazotekelezwa katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
Maudhui ya hija kama nembo ya umoja katika ulimwengu wa Kiislamu, falsafa ya hija, amani halisi katika kivuli cha hija na masharti ya Kiislamu ya kuhiji ni miongoni mwa masuala mengine yatakayojadiliwa katika vikao hivyo.
Vikao hivyo vimepangwa kufanyika tarehe 18 Septemba, 2, 16 na 30 za mwezi Oktoba mwaka huu katika kituo cha wasanii mjini Paris, kuanzia saa nne na nusu hadi saba na nusu kwa wakati wa Ufaransa.
Wanazuoni wa Kiislamu na walimu wa vituo vya Kiislamu nchini Ufaransa watakuwa na jukumu la kuwafundisha Waislamu wa nchi hiyo wanaokusudia kuhiji mwaka huu huko Makka. 649206
captcha