Hayo yamesemwa na Sayyid Mohammad Baqir mwakilishi wa Marajii Taqlid wa Kishia huko Kuwait. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sayyid Baqir ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kishia nchini Kuwait ameongeza kuwa waliotekeleza mashambulizi ya Septemba 11 hawakuwa Waislamu bali walikuwa magaidi ambao wanaendelea kumwaga damu ya watu wengi wasio na hatia. Amesema Maulamaa wa Kishia na Kisuni duniani walilaani hujuma hizo za kigaidi.
Sayyid Baqir ameongeza kuwa Wamarekani wenye misimamo mikali wanaoichoma moto Qur'ani wanataka kuzusha mapigano ya kidini.
652791