IQNA

12:44 - September 26, 2010
Habari ID: 2001498

Kiongozi wa Kanisa la Kopti la Misri akemea matamshi ya dharau dhidi ya Qur'ani

Mkuu wa kanisa la Kopti la Misri amelaani matamshi ya dharau yaliyotolewa hivi karibuni na kasisi mmoja wa nchi hiyo dhidi ya Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa gazeti la al-Misr al-Yaum, Papa Shenouda III amekuwa akiwasiliana na viongozi wa kidini na kisiasa wa Misri ili kupunguza athari mbaya za matamshi ya Kasisi Deir Al Anba Bishoy dhidi ya Qur'ani.
Madai ya kasisi huyo ya kuwepo aya iliyoongezwa kwenye Qur'ani Tukufu yameamsha hasira ya maulama, wanafikra na viongozi wa Kiislamu wa Misri ambao wametaka kasisi huyo achukuliwe hatua za kisheria.
Mawakili wa Misri pia wametoa taarifa wakitaka kasisi huyo atiwe nguvuni kutokana na matamshi yake hayo ya dharau dhidi ya Qur'ani. Baada ya kuona kuwa mashinikizo yameongezeka dhidi yake, kasisi Bishoy amedai kuwa hakuwa na lengo la kukosoa Qur'ani bali alikuwa na nia tu ya kuuliza swali kuhusiana na aya moja aliyodai kuwa iliongezwa kwenye Qur'ani baada ya kuaga dunia Mtume Mtukufu (saw) na katika kipindi cha utawala wa khalifa wa tatu, aya ambayo alihisi kuwa inagongana na itikadi za Kikristo. 662386
captcha