IQNA

21:13 - September 26, 2010
Habari ID: 2001883

Azerbaijan yataka kuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa OIC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Azerbaijan amekutana na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na kutaka mkutano ujao wa jumuiya hiyo ufanyike nchini Azerbaijan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Azerbaijan Elmar Mammadyarov amesema kuwa kufanyika mkutano kama huo nchini kwake kutazidisha ushawishi wa OIC katika nchi za kandokando ya Bahari ya Caspian na Bahari Nyeusi na pia katika nchi za Urusi ya zamani.
Vilevile amezitaka nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu kuunga mkono pendekezo la kufanyika mkutano wa jumuia hiyo nchini Azerbaijan.
Mkutano ujao wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu umepangwa kufanyika mwaka 2014.
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC iliundwa mwaka 1969 mjini Jeddah Saudi Arabia na inahesabiwa kuwa jumuiya kubwa zaidi ya kimataifa baada ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa na nchi wanachama 57. :662965

captcha