IQNA

13:05 - October 21, 2010
Habari ID: 2017021

ISESCO yatiliana saini mkataba na Kamati ya Kimataifa ya Elimu na Utamaduni ya ulimwengu wa Kiislamu

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, limetiliana saini huko Malaysia mkataba wa ushirikiano na Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kielimu na Utamaduni ya Umoja huo.

Mkataba huo ulitiwa saini katika kikao cha tano cha Mawaziri wa Elimu ya Juu wa nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC huko Kuala Lumpur Malaysia. Kwa mujibu wa mkataba huo, mashirika mawili hayo ya OIC katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2011 yatashirikiana kwa karibu katika nyanja za elimu na utamaduni ikiwemo tiba, sayansi ya anga, teknolojia ya kisasa, usimamizi wa maji na elimu ya mawasiliano na kilimo katika nchi za Kiislamu. 679242
captcha