Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, kongamano hilo litahudhuriwa na wanazuoni na wahadhiri kutoka vyuo vikuu kadhaa vya Ulaya pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari vya Uswisi, Marekan, Uholanzi, Ubelgiji, Uingereza, Denmark pamoja na taasisi kadhaa za utafiti.
Mufti wa Misri Sheikh Ali Gomaa anatazamiwa kutoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo. Hotuba yake italenga masuala ya mazungumzo baina ya wafuasi wa dini mbalimbali na onyo kuhusu uwezekano wa kutokea migongano baina ya staarabu.
682373