IQNA

14:57 - November 06, 2010
Habari ID: 2026377

Wazayuni wawazuia Waislamu wa Palestina kwenda hija

Kamati ya mateka wa Palestina imetangaza kuwa utawala ghasibu wa Israel umewazuia makumi ya Waislamu wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi kuelekea Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya hija.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Mateka wa Kipalestina imesema kuwa askari wa utawala ghasibu wa Israel wanawasimamisha Wapalestina wanaoelekea Makka katika mpaka wa Jordan na kupekua mizigo na masanduku yao.
Taarifa hiyo imesema kuwa baadhi ya Wapalestina hao wanazuiwa kuendelea ya safari ya hija kwa kisingizio kuwa ni hatari kwa utawala ghasibu wa Israel au kwa sababu eti za kiusalama.
Kamati ya Mateka wa Kipalestina imelaani mwenendo mbaya wa askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wanaotaka kuelekea Makka kwa ajili ya ibada ya hija na kusisitiza kuwa madai yanayotolewa na utawala huo kuhusu masuala ya kiusalama ni visingizio vya kuwazuia Wapalestina kwenda kutekeleza ibada ya hija. 689441
captcha