IQNA

15:08 - November 07, 2010
Habari ID: 2027179

Mpango wa kutoa mafunzo ya hija kwa mahujaji waanza kutekelezwa Makka

Mkoa wa Makka nchini Saudi Arabia umeanza kutekeleza mpango wa siku kumi wa kuwaelimisha mahujaji sheria za msimu wa hija kwa shabaha ya kukabiliana na changamoto zinazowasumbua askari usalama wa mji huo mtukufu katika siku za ibada ya hija.

Gazeti la Saudi Gazette limeandika kuwa changamoto kubwa zaidi zinazowakabili askari usalama wa Saudi Arabia katika msimu wa hija ni baadhi ya madereva kutoheshimu sheria za barabarani, kupakia abiria kupita kiasi kinachoruhusiwa, baadhi ya mahujaji kulala mitaani na kutekeleza ibada ya hija bila ya kuwa na kibali rasmi. Gazeti hilo limeandika kuwa mpango wa kuwaelimisha mahujaji unafanya jitihada za kuondoa matatizo hayo.
Abdul Rahman bin Khalaf ambaye ni miongoni mwa maafisa wanaotekeleza mpango huo anasema kuwa mahujaji wanaoishi katika mitaa ya maeneo ya hija wanasababisha matatizo kwa mahujaji kwa kufunga njia za maeneo hayo.
Amewataka mahujaji kufuata sheria za hija na kuwasiliana na polisi usalama pale wanapokabiliwa na tatizo lolote.
Ameongeza kuwa timu mbalimbali zimesambazwa katika maeneo ya mji wa Makka kwa ajili ya kugawa daftari zenye mwongozo na sheria za hija kwa mahujaji. 690177
captcha