Gerhard Wolf Mkurugenzi wa Utafutaji Masoko katika shirika kubwa la Ulaya la kuzalisha kakaratasi la Delfortgoup mjini Austria ameliambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA, kwamba, 'tunafuatilia kwa karibu suala la kuongezeka maombi ya uchapishaji Qur'ani Tukufu'.
Akizungumza pambizoni mwa mashindano na maonyesho ya uchapishaji misahafu yaliyofanyika mjini Tehran Wolf ameongeza kuwa, 'kiwango cha maombi ya kuchapishwa Qur'ani Tukufu kimeongezeka zaidi ya Bibilia'. Amesema kwa kuzingatia kuwa idadi ya Waislamu duniani imepindukia Bilioni 1.7 na inazidi kuongezeka, kuna haja ya kuongeza vituo vya kuchapisha misahafu.
Mashindano na maonyesho ya uchapishaji misahafu yalimalizika siku ya Jumatano mjini Tehran.
693256