Kwa mujibuwa wa tovuti ya ISESCO, al Tuwaijri katika ujumbe wake amesema umma wa Kiislamu unahitajia umoja na mshikamano zaidi kupitia kujiepusha na mifarakano. Amesema umoja utauwezesha umma wa Kiislamu kufikia malengo yake.
Katibu Mkuu wa ISESCO pia ameashiria nutka zinazowakutanisha pamoja za Waislamu wote katika fremu ya johari ya dini tukufu ya Kiislamu, Qur'ani na Qibla na kusisitiza kuwa, 'mifarakano inaenda kinyume na mafundisho ya Qur'ani na kudhoofisha umma wa Kiislamu.
Kuhusu kadhia ya Palestina, mkuu huyo wa ISESCO amesema kuna haja ya kuwepo umoja miongoni mwa makundi ya Wapalestina ili waweza kukabiliana na uhasama wa utawala wa Kizayuni. Aidha ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuwasaidia watu wa Palestina katika kukabiliana na Wazayuni. al Tuwaijri amesema, 'kukombolewa Quds Tukufu na ardhi zote za Palestina ni wadhifa mtakatifu na asili wa umma wa Kiislamu.
695582