Muswada huo unalenga kuzuia vitendo na harakati zote za watu au makundi yanayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu na dini nyingine.
Kituo cha habari cha “risalehaber” kimeripoti kuwa muswada huo utajadiliwa wiki ijayo katika Baraza Kuu licha ya upinzani mkubwa wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya.
Mwakilishi wa OIC katika Umoja wa Mataifa Ufuk Gökçen amesema kuwa kisingizio kinachotumiwa na nchi zinazopinga kupasishwa muswada huo ni kuwa unaweza kutumiwa kwa ajili ya kuziwekea mashinikizo jamii za dini zenye wafuasi wachache. Amesema kuwa kisingizio hicho hakina msingi wowote.
Ameongeza kuwa kikao cha wiki ijayo cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ndio fursa pekee ya kuweza kupasishwa muswada huu kwa mwaka huu wa Miladia na OIC inafanya jitihada za kuzishawishi nchi mbalimbali zipasishe muswada huo unaopiga marufuku vutendo na harakati zinazovunjia heshima matukufu ya dini mbalimbali.
Muswada huo unaopiga marufuku vitendo na harakati zinazovunjia heshima matukufu ya dini mbalimbali ulipasishwa na Umoja wa Mataifa tarehe 26 Machi licha ya upinzani mkubwa wa Marekani na nchi za Ulaya lakini hadi sasa haujapata nguvu ya kuwa sheria inayopaswa kutekelezwa na nchi wanachama. Kwa msingi huo Jumuiya ya Nchi za Kiislamu inafanya jitihada za kuhakikisha kwamba Umoja wa Mataifa unapasisha makubaliano ya kimataifa ya kupiga marufuku vitendo na harakati zote zinazovunjia heshima dini mbalimbali. 695536