Habari hiyo imetangazwa na Naibu Katibu wa Jumuiya ya Kiislamu ya America ya Latini Hussein Awadh ambaye amezitaka nchi Kiislamu kusaidia ujenzi wa kituo hicho.
Amesema kuwa kutokuwepo maimamu wa misikiti na wahubiri wa Kiislamu wanaozungumza vyema lugha ya Kihispania ni tatizo kubwa zaidi linalotatiza shughuli za ulinganiaji wa Kiislamu katika nchi za America ya Latini.
Ameashiria nafasi muhimu ya jumuiya za Kiislamu katika kuarifisha Uislamu na kusahihisha sura isiyokuwa sahihi inayoenezwa na Wamagharibi kuhusu dini hiyo na akasema kuwa wahubiri wa Kiislamu wanaoelewa hali ya dunia ya sasa wanaweza kubainisha mitazamo ya Uislamu kuhusu masuala mbalimbali na pia thamani za dini hiyo kupitia njia ya kutoa hotuba katika minasaba mbalimbali. 700340