Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu anayeshughulikia masuala ya Palestina Muhammad Sabih amelaani vitendo hivyo na kusema kuwa jinai za Wazayuni za kuharibu nyumba za Wapalestina zimawalazimisha raia wengi wa eneo la al Aghwar kubakia bila ya makazi.
Amesisitiza kuwa siasa za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina zimepita jinai za Makaburu na wabaguzi wa rangi wa Afrika Kusini.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amezitaka nchi mbalimbali, jumuiya za kiraia, taasisi za kutetea haki za binadamu na jamii ya kimataifa kwa ujumla kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Israel huko Palestina na kukomesha ukatili wake dhidi ya raia wasiokuwa na hatia. 702746