Kongamano hilo litasimamiwa na sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ikishirikiana na jumuiya na taasisi 24 za Kimataifa za Kiislamu.
Mada kuu ya kongamano hilo ni changamoto zinazowakabili Waislamu waliowachache Ulaya mashariki na kati na mchango wao katika mwenendo wa ustawi endelevu katika nchi zao.
Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu imetangaza kuwa maudhui nyingine za kongamano hilo ni pamoja na uchunguzi kuhusu fursa na changamoto zinazozikabili jamii za Kiislamu katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na mchango wa jumuiya za Waislamu katika kupambana na hujuma na propaganda chafu za kuwatisha watu na Uislamu. 703653