IQNA

21:18 - December 04, 2010
Habari ID: 2042063

Mwakilishi aliyeuvunjia heshima Uislamu atozwa faini

Mahakama ya Copenhagen imemhukumu adhabu ya kutoa faini ya Krone elfu tano mwakilishi wa chama chenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia nchini Denmark kutokana kuukashifu Uislamu.

Kasisi Jesper Marquard Langballe mwenye mfungamano na serikali ya Denmark na mbunge wa Chama cha Wananchi amehukumiwa adhabu ya kutoa faini ya Krone elfu tano kwa kukiuka kifungu cha 266 cha Katiba ya Denmark kinachopiga marufuku kutoa matamshi ya kibaguzi na kuwavunjia heshima raia kutokana na mbari, rangi, dini na lugha zao.
Mbunge huyo mwenye misimamo ya kuchupa mipaka ameutuhumu Uislamu kwamba hauzingatii familia na kwamba unamdhalilisha mwanamke.
Katika miezi ya hivi karibuni Bunge la Denmark lilifanya vikao vya dharura na kuwataka viongozi wa mahakama za nchi hiyo kusimamisha kesi ya mbunge huyo. Hata hivyo mahakama ya Copenhagen imekataa ombi hilo na kumfikisha mahakamani. 705915
captcha