Kitabu hicho kilichoandikwa kwa Kiingereza na hayati Ahmad Deedat msomi wa Afrika Kusini kimetarjumiwa kwa Kihausa na mfasiri Muislamu kutoka Nigeria Mohammad Sani Abubakr .
Kitabu hicho kimechapishwa kwa lengo la kuwaelimisha wanaozungumza lugha ya Hausa kuwa kubaathiwa Mtume wa Uislamu (SAW) kumebashiriwa katika kitabu kitakatifu cha Wakristo.
Wahubiri Wakristo wamekuwa wakieneza propaganda potofu za dini yao miongoni mwa Wahausa ambao aghalabu ni Waislamu na hivyo kitabu hicho kinasisitiza kuwa Mtume Muhammad SAW ndio Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.
Mfasiri wa kitabu hicho anaamini kuwa kitaweza kufafanua zaidi ukweli wa Uislamu na kwamba kinatoa majibu kwa maswali mengi kuhusu suala la Utume.
720290