Mashindano haya yatafanyika kwa njia ya mtandao, yakiratibiwa kutoka mji wa Fez, nchini Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi hiyo, jumla ya washiriki 117, wakiwemo wanawake 13, wanatarajiwa kushiriki. Washiriki hao watashindana katika makundi matatu:
Kuhifadhi Qur’ani yote na kusoma kwa qira’a ya Warsh kutoka kwa riwaya ya Nafi‘.
Kuhifadhi Qur’ani yote na kusoma kwa qira’a nyinginezo.
Tajwidi sambamba na kuhifadhi angalau Juzuu tano za Qur’ani.
Kamati ya majaji itajumuisha maulamaa na wasomaji wa Qur’ani kutoka Morocco, Mauritania, Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Nigeria, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan, Ethiopia, Tanzania, na Somalia. Watafanya tathmini ya washiriki wakiwa mjini Fez.
Timu ya kiufundi mjini Fez, kwa ushirikiano na matawi ya taasisi hiyo barani Afrika, itasimamia urushaji wa mashindano hayo kupitia jukwaa la Zoom.
Mashindano haya ni utekelezaji wa mapendekezo ya mwaka 2018 kutoka Baraza Kuu la Taasisi ya Mfalme Mohammed VI ya Maulamaa wa Afrika, lililopendekeza kufanyika kwa mashindano ya kila mwaka ya Qur’ani. Matoleo yaliyopita yalifanyika kwa ushirikiano na matawi 48 ya taasisi hiyo barani Afrika, kila tawi likiandaa duru za awali za kuchuja washiriki wa fainali.
Taasisi hiyo imesema lengo kuu la mashindano haya ni kuimarisha uhusiano wa vijana Waislamu wa Afrika na Qur’ani Tukufu, sambamba na kuhamasisha kuhifadhi na kusoma kwa ufasaha Kitabu hicho kitukufu.
3494674