IQNA

Kuakisiwa shughuli za Isesco katika jarida la Argentina

12:36 - January 01, 2011
Habari ID: 2056406
Katika toleo lake la hivi karibuni jarida la El Mundo Arabe la Argentina limechapisha makala ya shughuli za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Katika makala hiyo Jarida hilo limezungumzia kwa kina kuhusu shughuli za ISESCO, nafasi ya shirika hilo katika ulimwengu wa Kiislamu na pia nafasi ya Abdul Aziz Othman at-Tuwaijri, katibu Mkuu wa jumuiya hiyo katika kufikia malengo yake.
Maudhui nyingine iliyojadiliwa katika jarida hilo linalochapishwa huko Buenos Aires mji mkuu wa Agentina, ni vijana wa Kiislamu na mabadiliko katika vyanzo vya masomo na athari ya Ulaya katika ulimwengu wa Kiarabu, makala ambazo zimeandikwa na Katibu Mkuu wa ISESCO.721460
captcha