IQNA

13:13 - January 03, 2011
Habari ID: 2057892

Mwajilishi wa Mamarja' nchini Kuwait alaani mlipuko wa kigaidi wa Alexandria

Muhammad Baqir al-Musawi al-Muhri, mwakilishi wa Mamarja' nchini Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Kikristo la nchi hiyo Jumamosi ametoa taarifa akilaani vikali shambulio la bomu la hivi karibuni pembeni ya kanisa moja huko katika mji wa Alexandria nchini Misri.

Watu wapatao 21 wakiwemo Waislamu, wanaripotiwa kuuawa na wengine 70 kujeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea karibuni na kanisa la Makopti la al-Qiddissin. Amesema mlipuko huo hauna tafsiri nyingine isipokuwa ni ugaidi wa moja kwa moja ambao unapasa kulaaniwa na duru zote za kimataifa, Kiislamu na kiutu. Ametoa mkono wa pole kwa Papa, Vatican, watu wa Misri na Wakristo wote duniani kutokana na mlipuko huo na kumuomba Mwenyezi Mungu alipize kisasi dhidi ya magaidi waliohusika na kitendo hicho ambacho amesema kinakwenda kinyume kabisa na thamani pamoja na mafundisho ya Kiislamu.
Sayyid Baqir al-Muhri amezitaka taasisi, jumuiya, vyama, harakati na wanazuoni walio na misimamo ya wastani kulaani vikali vitendo kama hivyo vya kigaidi popote vinapotokea duniani. Jumuiya ya Wanazuoni na Wanafikra wa Palestina pia imetoa taarifa ikilaani kitendo hicho cha kigaidi na kusema kuwa kiko nje ya mafundisho na tahamani sahihi za Kiislamu. 722844
captcha