Taarifa ya jumuiya hiyo imesema utawala wa Kizayuni unaendeleza sera zake za ubomoaji na usambaratishaji maeneo yenye umuhimu wa kiutamaduni na kimaanawi ya Wapalestina. Taarifa hiyo imesema sera hizo za kibaguzi zinazusha swali kubwa kuhusu sula la kuheshimu Utawala wa Kizayuni maazimio ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unawalazimisha Wapalestina kufuata sheria za umiliki wa mali kinyume cha sheria za kimataifa.
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni na taasisi zinginezo kuchukua hatua imara kuzuia ukiukwaji wa sheria unaofanywa na utawala wa Kizayuni.
Aidha nchi za Kiarabu zimetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kuzuia jinai za utawala wa Kizayuni.
727677