IQNA

Kitabu cha “Imam Mahdi (as) kwa Ahlul Sunna” chachapishwa tena

13:41 - January 10, 2011
Habari ID: 2062086
Kitabu cha Imam Mahdi (as) katima Mtazamo wa Ahlul Sunna” kilichoandikwa na Mahdi Faqih Imani kimechapicha kwa mara ya tatu katika mji mkuu wa Lebanon, Beiruti kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait.
Maudhui za kitabu hicho zinajumuisha uchunguzi kuhusu itikadi ya kuwepo Imam Mahdi (as), kuzaliwa na maisha yake, kwenda kwake ghaiba ndogo, ghaiba kubwa, hali ya wakati wa kudhihiri kwake, wafuasi wake kwa mujibu wa itikadi na mafundisho ya Ahlul Bait (as) na kadhalika.
Mwandishi wa kitabu hicho amekusanya maudhui kuhusu kuzaliwa kwa Imam Mahdi (as), kughibu na kudhihiri kwake kutoka katika vitabu vya Kisuni.
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait imeamua kuchapicha tena kitabu hicho kwa mara ya tatu kutokana na umuhimu wa maudhui zake. 727387
captcha