Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kuwa maonyesho hayo ya sanaa yaliyoanza Alkhamisi iliyopita kwa usimamizi wa Wasanii Wasio na Mpaka yataendelea kwa kipindi cha wiki mbili.
Mabango 40 ya maonyesho hayo yanaakisi mashaka ya watoto wadogo wa Palestina na mengine thalathini ni ya kazi za wasanii mashuhuri wa Uhispania na Ufaransa yanayozungumzia maudhui mbalimbali kuhusu watoto wa Kipalestina.
Vilevile shirika la habari la Palestina limeripoti kuwa mwanachama wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi wa Palestina UNRWA Rachel Marty amesema kuwa maonyesho hayo yana lengo la kuonyesha umuhimu wa kadhia ya Palestina na mashaka yanayowapata wakimbizi wa Kipalestina hususan watoto wadogo. 730544