IQNA

Msikiti wa Abu Dhabi, watembelewa na wageni laki tatu mwezi Disemba

13:16 - January 17, 2011
Habari ID: 2066032
Watu wanaovutiwa na masuala ya sanaa wapatao laki tatu waliutembelea Msikiti wa Sheikh Zayed wa mjini Abu Dhabi mwezi uliopita wa Disemba.
Kwa mujibu wa gazeti la Khaleej Times linalochapishwa nchini Imarati, msikiti huo huwa wazi tokea saa tatu asubuhi hadi mbili usiku kwa saa za Imarati kwa ajili ya kuwakaribisha wageni wanaovutiwa na masuala ya sanaa ya Kiislamu.
Wakiwa msikitini humo, wageni hubainishiwa masuala mbalimbali yanayohusiana na sanaa na usanifu majengo wa Kiislamu pamoja na mbinu zilizotumika katika ujenzi wa msikiti huo unaowavutia wageni wengi kila mwaka na uliojengwa mwaka 1996 kwa amri ya Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan.
Msikiti huo hutembelewa kila siku na wageni wengi Waislamu na wasio Waislamu wanaovutiwa na sanaa ya Kiislamu. 731079
captcha