Hayo yamesemwa na msanifu majengo maarufu Ibrahim Muhammad Jaidah alipohutubia awamu ya pili ya "Mijadala ya Kijani ya Doha" DGD. Mjadala wa mwaka huu umefanyika mjini Doha Qatar chini ya anwani ya "Nyumba za Kijani kwa Mtazamo wa Kiislamu na Kiusanifu Majengo"
Jaida amesema kuwa maendeleo ya miji ya nchi za Kiislamu hayaakisi sanaa ya Kiislamu ya usanifu majengo kama ilivyokuwa huko nyuma.
Ameelezea namna usanifu majengo wa kale wa miji ya Kiislamu ulivyozingatia masuala ya uchumu na mazingira.
"Kaaba, nyumba ya kwanza iliyochaguliwa na Nabii Ibrahim AS iliakisi usahali katika usanifu majengo wa Kiislamu. Al Madina, mji wa kwanza wa Kiislamu pia ni mfano wa kuigwa" amesema msomi huyo.
Jaida amesema kuwa miji ya kale ya Kiislamu kama vile Quds , Damascus, Cairo na Istanbul ilijengwa kwa kuzingatia mazingira pamoja na mila na desturi za Waislamu wa miji hiyo.
732039