Tovuti ya Islam Today imeripoti kuwa maonyesho hayo yaliyoanza tarehe 11 Januari yana kazi na athari za msanii marufu wa Kiislamu wa Ujerumani Michael Claus Smith.
Smith amesema kuhusu maonyesho hayo kwamba ametayarisha kazi za sanaa ya Kiislamu na Kimarekani. Ameongeza kuwa kazi hiyo ya kisanii ni mseto wa misingi ya Kiislamu na mbinu yake makhsusi ya usanii.
Kazi za kisanii za Smith zilionyeshwa hivi karibuni katika maonyesho ya kimataifa ya wasanii Waislamu huko New Orleans Marekani na katika mji wa al Khubar nchini Saudi Arabia.
Maonyesho ya sasa ya sanaa za Kiislamu mjini Illinoise yataendelea hadi tarehe 11 Februari. 733336