Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kitabu hicho kimeandikwa na Christopher Weeramatnry Mkuu wa Zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ ambaye aliwahi kuwa jaji katika Mahakama Kuu ya Sri Lanka. Tafsiri ya Kiarabu ya kitabu hicho iliyopewa jina la Al-Fiqh Al-Islami Min Mandouril Alami imetayarishwa na Dr. Ahmed el Alaoui.
Kitabu kingine ambacho kimechapishwa na ISESCO hivi karibuni ni " Asalat Al-Madrassa Al-Malikia Al Fasia' yaani 'Chimbuko cha Shule ya al Malikia ya Fez' nchini Morocco.
Kitabu hicho kimechapishwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Morocco na ISESCO kwa mnasaba wa mji wa Fez kuwa Mji Mkuu wa Utamaduni wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu mwaka 2007.
733570